Mbunge Mathayo Kuongeza michezo mashindano ya jimbo Cup
MBUNGE wa jimbo la Musoma
mjini, Vedastus Mathayo (CCM), ameongeza michezo zaidi kwenye mashindano ya
Jimbo yatakayofanyika baadae mwaka huu na kuzitaka Kata 16 zinazounda jimbo
hilo kuanza kujiandaa kushiriki na kujipatia zawadi mbalimbali.
Akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Mshikamano, alisema mwaka huu
mashindano anayoandaa yataendelea kama kawaida na yataboreshwa zaidi kwa
kuongeza michezo mingi tofauti na ilivyokuwa kwenye mchezo wa soka pekee.
Amesema licha ya mchezo
wa soka lakini pia kwa mwaka huu kutakuwa na mchezo wa mpira wa
pete,riadha,kupiga makasia kwenye mitumbwi,drafti,darts,kukimbia kwenye magunia
pamoja na kufukuza kuku na kutoa wito kwa kila mmoja kujiandaa.
Mathayo alisema michezo
ni kitu ambacho kwa upande wake anakipenda na kudai mara baada ya kuifanikisha
timu ya Biashara United kucheza ligi kuu msimu ujao sasa ni zamu ya wananchi
wote wa jimbo la Musoma mjini kupata burudani ya kila mchezo pamoja na zawadi.
Alisema kila Kata itapata
jezi pamoja na mipira kwaajili ya kuzitumia kwenye mashindano hayo na
maandalizi na mipango ya kufanyika kwa mashindano hayo inakwenda vizuri ili
kuyafanya mashindano hayo kuwa na nguvu kubwa.
“ Vijana naomba mjiandae
kwaajili ya mashindano ya jimbo na mwaka huu kutakuwa na michezo
mingi na kila mchezo utakuwa na zawadi yake kikubwa muanze maandalizi na
naamimi madiwani wa kila Kata wataziandaa timu vizuri.
“ Mwaka huu sio vijana tu
hata wazee wetu watashiriki maana kutakuwa na mashindano ya drafti na kukimbia
kwenye magunia pamoja na darts naamini huko wazee wetu hawatakosekana nao pia
watapata zawasi kupitia mashindano hayo,”alisema Mathayo.
Diwani wa Kata ya Nyasho
ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Haji Mtete (CCM), alisema Mathayo
amekuwa akichangia kuinua michezo katika mji wa Musoma kupitia mashindano ya
jimbo na anastahili kuungwa mkono na wadau wengine.
Nao vijana walioshiriki
mkutano huo wamefarijikia na kusikia ujio wa mashindano hayo na kudai
watajiandaa mapema ili kuweza kushiriki mashindano hayo na kupata zawadi
zitakazotolewa na mbunge huyo kwa washindi.
Mathayo akiwa na wachezaji wa timu ya Biashara walipokuwa kwenye mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma |
No comments