Wazee Musoma wamtuma Mathayo kukutana na wabunge wa mkoa wa Mara

 BARAZA la wazee wa manispaa ya Musoma wamemtuma mbunge wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo, kukutana na wabunge wanaotoka mkoa wa Mara bila kujali itikadi zao za vyama kupanga ajenda moja ya kuchangia kwa pamoja na kufatilia miradi ya maendeleo ya mkoa wa Mara katika vikao vya bunge la bajeti litakaloanza mwezi ujao.
 Wakizungumza kwenye kikao cha pamoja na mbunge huyo,wazee hao wamesema zipo ajenda ambazo bila kuzizungumza kwa pamoja kwa maendeleo ya mkoa wa Mara haziwezi kupita kwa haraka hivyo ni muhimu wabunge hao wakawa kitu kimoja na kuchangia hoja kutokana na umoja wao.
 Mwenyekiti wa baraza hilo, Enock Ruyembe, amesema mbunge Mathayo amefanya jambo la msingi kukutana nao na jambo la msingi wanalomuagiza kabla ya vikao vya bajeti ni kukutana na wabunge wote wa mkoa wa Mara na kuwa na kauli moja katika kuchangia mijadala mbalimbali kwa maendeleo ya mkoa wa Mara
 Akizungumza kwenye kikao hicho, mbunge wa Jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo, amesema wabunge wa mkoa wa Mara tayari wanao umoja wao chini ya Mwenyekiti wao Profesa Sospeter Muhongo na mawazo waliyoyatoa atayapeleka kwa wabunge wenzake.
 Mathayo amesema ni utaratibu wake kukutana na makundi mbalimbali kabla ya kwenda kwenye vikao vya bunge kupeleka mawazo ya wananchi na ameshafanya hivyo kabla ya kuanza kwa vikao vya bajeti vitakavyoanza mwezi ujao.


No comments

Kamati zapewa mafunzo ya kupambana na ukatili

KAMATI za kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya wilaya ya Rorya zimepewa mafunzo ya kupambana na masuala ya ...

Powered by Blogger.