Kamati zapewa mafunzo ya kupambana na ukatili
KAMATI za
kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya wilaya ya
Rorya zimepewa mafunzo ya kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia ili
ziweze kufanya kazi na kutolea taarifa vitendo vyote vya ukatili.
Mafunzo hayo
yametolewa kwenye kamati hizo ukiwa ni mwendelezo wa elimu kwenye makundi
mbalimbali yanayotolewa na shirika la Masister wa Moyo Safi wa Maria (Baraki
Sisters Farm) kwa ufadhili wa shirika la The Foundation For Civil Society.
Akizungumza
wakati wa utoaji wa mafunzo hayo, Mratibu wa mafunzo hayo, ,Nollasco Mgimba,
amesema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa kamati za ulinzi wa wanawake na
watoto na zitawasaidia katika utoaji wa taarifa.
Amesema
ukatili unaanzia kwenye familia na mafunzo hayo yamelenga namna ya utoaji wa
taarifa na yamewashirikisha jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia ambao
wamesaidia kutoa muongozo namna ya utoaji wa taarifa pale wanapoona matukio ya
ukatili.
Wakizungumza
mara baada ya kupokea mafunzo hayo, wanakamati hao kutoka vijiji mbalimbali vya
wilaya hiyo wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika utoaji wa taarifa maana
kabla ya kupokea mafunzo hayo walikuwa hawana uelewa wowote.
No comments