Madiwani watoa onyo kali kwa watumishi manispaa ya Musoma



BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Musoma limetoa barua za onyo kali kwa watumishi 6 wa halmashauri hiyo kwa kushindwa kuhudhuria vikao vya baraza hilo na vile vya kamati mbalimbali bila kutoa taarifa yoyote na kushindwa kupatikana majibu ya hoja zinazo wahusu.

Akizungumza kwenye baraza hilo mara baada ya baraza kujigeuza kama kamati kuwajadili watumishi hao kutoka kwenye idara za ardhi,afya na mazingira, meya wa manispaa hiyo,Patrick Gumbo, amesema watumishi wasiofuata taratibu za vikao hawawezi kuvumiliwa kutokana na umuhimu wa vikao wanavyostahili kuwepo.
Amesema  kwenye vikao hivyo vya baraza na kamati zipo hoja ambazo zinastahili kujibiwa na watumishi hususani wakuu wa idara hivyo kukosekana kwao kunapelekea ugumu wa maamuzi ya vikao na kupata uufumbuzi wake.
Gumbo amesema wapo watumishi ambao wanafika kwenye vikao na kuandika mahudhurio kisha kuondoka na wapo ambao hawafiki kabisa na madiwani kama wasimamizi wa halmashauri hawakubaliani na jambo hilo.

Amesema  baraza limeamua kutoa barua za onyo kali kwa watumishi hao na pale watakapoendelea na tabia hizo hawatasita kuwachukulia hatua nyingine kwa mujibu wa taratibu na kanuni zinazowaongoza.
“ Haiwezekani madiwani wanafika kwenye vikao lakini watumishi wanaotakiwa kujibu baadhi ya hoja zinazotolewa wanakuwa hawapo kwenye vikao hili halikubaliki lazima tuzingatie taratibu,”amesema Gumbo.
 Diwani wa viti maalum, Amina Masisa akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani
 madiwani wakijadiliana jambo
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Musoma mjini, Magiri Bendictor(kulia) akiwa na Katibu wa wilaya hiyo Benard Ghaty kwenye baraza hilo
 Mkurugenzi wa manispaa ya Musoma, Fedrica Myovella,akizungumza kwenye kikao hicho cha baraza
 Diwani wa Kata ya Nyasho, Haji Mtete akifatilia kikao hicho

 Diwani  wa Kata ya Kitaji,Frenk Wabare,


No comments

Kamati zapewa mafunzo ya kupambana na ukatili

KAMATI za kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya wilaya ya Rorya zimepewa mafunzo ya kupambana na masuala ya ...

Powered by Blogger.