Wafanyakazi NSSF mkoa wa Mara waunga mkono kampeni ya mbunge Mathayo ujenzi wa madarasa
WAFANYAKAZI
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii ( NSSF) mkoa wa Mara wameunga mkono
juhudi za mbunge wa jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo, ya kampeni ya
kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari
manispaa ya Musoma ili kumaliza uhaba uliopo.
Katika kikao cha mbunge Mathayo na wafanyakazi hao kilichofanyika kwenye ofisi ya shirika hilo walichangia kiasi cha shilingi milioni moja laki nane na nusu na kudai huo ni mwanzo na wataendelea kushirikiana kwenye kampeni hiyo. Meneja wa NSSF mkoa wa MARA, Rashid Kwangaya, amesema kampeni iliyoanzishwa na mbunge Mathayo inapaswa kuungwa mkono na kila mmoja ili lengo lililokusidiwa liweze kufanikiwa. Kwa upande wake Mbunge Mathayo, amewashukuru wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Mara kwa namna walivyoguswa na kuamua kuchangia ili kuweza kupunguza na kumaliza tatizo la vyomba vya madarasa ambapo vinahitajika vyumba zaidi 500. |
Picha tofauti wafanyakazi wa NSSF mkoa wa Mara wakifatilia kikao hicho |
No comments