Chanjo ya saratani kwa watoto wa kike Mara kuanza aprili 23 hadi 30
Zoezi la chanjo ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike wenye umri chini ya miaka 14 inatarajiwa kuanza aprili 23 hadi 30 mwaka huu ambapo inatarajia kuanza kwenye wilaya zote za mkoa wa Mara huku watoto zaidi ya elfu 30 wakitarajiwa kupatiwa chanjo hiyo.
Mratibu wa chanjo mkoa wa Mara, Dk. Lukona, amesema maandalizi yote ya zoezi hilo ambalo kitaifa limeshazinduliwa na Makamu wa Rais, kwa mkoa wa Mara maandalizi yake yanakwenda vizuri na linatarajiwa kufanyika kwa ufanisi.
Amesema chanjo hiyo ni salama na haina madhara yoyote na serikali imeamua kuitoa bila gharama yoyote ili kuwalinda watoto hao baadae kuja kupata ugonjwa wa kansa ya saratani ya shingo ya kizazi.

Mganga mkuu wa mkoa wa Mara, Dk. Francis, amesema kama ambavyo chanjo nyingine zilifanikiwa zikiwemo za surua na pepopunda hata ya saratani kwa watoto wa kike itafanikiwa na kuwataka wananchi kuondoa wasiwasi na zoezi hilolitakapoanza waweze kutoa ushirikiano kwa wataalamu watakaokuwa wanaendesha zoezi hilo.
Akifungua mafunzo kwa wadau mbalimbali wa afya wakiwemo viongozi wa dini kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara,Adam Malima,mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano, amesema serikali ina nia njema na wananchi wake na chanjo hiyo ni salama na kutaka hamasa itolewe ili kila mlrngwa aliyekusudiwa kwenye chanjo hiyo aweze kuipata.
No comments