Muhongo awaongoza wananchi kuchangia mifuko 500 ya saruji kwa ujenzi wa zahanati
MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini,
Profesa Sospeter Muhongo, amewaongoza madiwani pamoja na wananchi wa jimbo hilo
kuchangia vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko 500 ya saruji,nondo na misumali
katika kukamilisha ujenzi wa zahanati na nyumba ya mganga katika vijiji vya
Kurwaki na Kigera Etuma.
Akizungumza mara baada ya kuendesha
zoezi hilo katika ziara yake ya siku 3 jimboni, alisema suala la afya za
wananchi ni suala muhimu ambalo ni moja ya vipaumbele vyake katika kuhakikisha
wananchi wanakuwa na afya njema ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli
za maendeleo.
Amesema adhima ya serikali ni
kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na zahanati kwaajili ya kuwapa huduma wananchi
nay eye kama mbunge anayewajali wananchi wake atahakikisha anatoa ushirikiano
unaohitajika katika kufanikisha na kupatikana huduma za afya kwenye kila eneo.
Muhongo ambaye alichangia zaidi ya
mifuko 300 kwenye zahanati ya vijiji hivyo pamoja na vifaa vingine vya
ujenzi,alisema wananchi pia wanapaswa kuchangia na sio kuisubilia serikali
kuwafanyia kila jambo huku wenyewe wakikaa pembeni.
Alisema bila kuwa na afya njema
mwananchi hawezi kushiriki shughuli za maendeleo hivyo kuendelea kuwa masikini
suala ambalo anapambana nalo kuhakikisha wananchi wanakuwa na uchumi mzuri na
kusomesha watoto.
“ Pamoja na kipaumbele kikubwa cha
elimu katika jimbo letu lakini afya ni suala la msingi ambalo tunapaswa
kulizingatia kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema na wanapata huduma za
afya katika maeneo yao ya karibu katika kuunga mkono juhudi za serikali.
“ Niwashukuru madiwani na wananchi
katika kuunga mkono juhudi hizi kwa kuchangia kadri mnavyoweza ili vijiji vyetu
viweze kupata zahanati na nyumba za waganga wanaotuhudumia maana bila kuwa na
afya njema hatuwezi kushiriki shughuli za maendeleo,”amesema Muhongo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Musoma,
Charles Magoma, amesema Muhongo amekuwa akifanya juhudi kubwa katika shughuli
za maendeleo na katika zahati tayari ameshachangia katika ujenzi wa zahanati 9
ambazo zinaendelea kujengwa ambazo zitasaidia kusogeza huduma kwa wananchi na
kuahidi kuendelea kumuunga mkono.
Diwani wa Kata ya Nyakatende, Rufumbo
Mgini, amesema Kata yake ambayo ina vijiji 4 ilikuwa haina zahanati hata moja
tangu kupata uhuru rakini jitihada za mbunge Muhongo zimefanikisha kupatikana
kwa zahanati katika Kijiji cha Kigera Etuma pamoja na nyumba ya Mganga hivyo
kuwapunguzia adha wananchi ya kutembea umbali waa kilometa
Akimalizia ziara yake kwenye Kata ya Nyegina, Muhongo aliwashukuru wananchi wa zawa wa Musoma vijijini kwenye maeneo ya Nyegina na Mkirira kwa kushirikiana kuchangia jumla ya shilingi milioni 1.6 na mifuko 238 ya saruji kwaajili ya zahanati ya Kijiji cha Mkirira ambapo jimbo limebuni mbinu mpya ya kushirikiana na serikali kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa kuwashirikisha wananchi walipo ndani na nje ya jimbo hilo.
No comments