Benki ya NMB yawaita wakulima wa pamba kufungua akaunt
BENKI ya NMB
wilayani Bunda imewaita wakulima wa zao la pamba kufungua akaunti kwenye benki
hiyo ili kuweza kupitiishiwa malipo yao ya ununuzi wa zao hilo katika msimu wa
ununuzi utakaonza mei mosi mwaka huu.
Akizungumza
kwenye mkutano wa utoaji elimu kwa wakulima kabla ya kuanza kwa msimu wa
ununuzi uliongozwa na mkuu wa wilaya ya Bunda, Lyidia Bupilipili, kwenye vijiji
vya Hunyari, Kiroleli na Nyamswa,meneja wa NMB tawi la Bunda,Antipas Nnko,
amesema wakulima wasiwe na wasiwasi na benki hiyo kwa kuwa fedha zao zitakuwa
sehemu salama.
Amesema
inayo fursa ya akaunti ya chapchap ambayo inafunguliwa bure na watawafata
wakulima kwenye maeneo yao na kinachohitajika ni kuwa na kitambulisho cha taifa
au barua ya utambulisho kutoka kwa mtendaji wa Kata.
Nnko amesema
wanunuzi wote wa pamba wanazo akaunt kwenye benki hiyo hivyo itakuwa rahisi
kuhamisha fedha kutoka akaunt moja kwenda akaunti nyingine kuliko kufungua
akaunt kwenye benki nyingine.
MKUU wa wilaya ya Bunda, Lyidia Bupilipili, akisisitiza umuhimu wa kufungua akaunt kwa kuwa malipo yote ya ununuzi wa pamba msimu huu yatapitia benki |
Kaimu meneja wa Wakala wa Vipimo mkoa wa Mara, Jacob Lyambo, akitoa elimu ya mizani kwenye mkutano na wakulima wa pamba wilayani Bunda
Wakulima wa pamba wakifatilia elimu enayotolewa
No comments