Mbunge Mathayo awataka mashabiki wa Biashara United kuondoa wasiwasi




MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo,ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ukarabati wa uwanja wa kumbukumbu ya Karume utakaotumiwa na timu ya Biashara United katika michezo ya ligi msimu ujao,amewaondoa shaka mashabiki wa timu hiyo kwa timu yao kuutumia uwanja huo.

Akizungumza kuhusana na maendeleo ya ukarabati wa uwanja amesema licha ya mvua kusumbua lakini wanapambana kuhakikisha unakamilika kabla ya ligi kuanza na mashabiki hao kupata nafasi ya kuiona timu yao ikiiutumia uwanja huo.


Amesema tayari wameanza kusambaza udongo na mbegu za nyasi zimeshafika kutoka afrika kusini na ziatarajiwa kupandwa kwa wakati na kuota kabla ya ligi kuu kuanza baadae mwaka huu.

Mathayo amesema viongozi mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele kufatilia maendeleo ya uwanja huo wakiwemo wabunge,mkuu wa mkoa,wamiliki wa uwanja huo Chama cha Mapinduzi pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanakamilika.



Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini, Profesa Sospeter Muhongo,amesema wako pamoja kuhakikisha uwanja huo unakamilika kwa wakati licha ya changamoto ya mvua zinazoendelea kunyesha


No comments

Kamati zapewa mafunzo ya kupambana na ukatili

KAMATI za kupambana na masuala ya ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya wilaya ya Rorya zimepewa mafunzo ya kupambana na masuala ya ...

Powered by Blogger.