Diwani Masumbuko awahamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja
wa shule ya msingi Nyamatare, Masumbuko amesema suala la afya ni mtambuka na ni
muhimu kila mwananchi akiwa na uhakika wa kupata huduma.
Amesema CHF iliyoboreshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) itamuwezesha mwananchi kupata huduma katika zahanati,vituo vya afya na
hospitali zilizopo mkoa wa Mara tofauti na mwanzo ambapo huduma zilikuwa
zikitolewa kwenye halmashauri moja.
Masumbuko amesema mwananchi anapokuwa na afya njema anapata
fursa ya kufanya shughuli za kiuchumi na kumuingizia kipato kitakacho muwezesha
kujikimu ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto.
Amesema baada ya kuboreshwa kwa huduma za afya kupitia CHF
itawapasa wananchi kuchangia shilingi elfu 30 badala ya elfu 10 na kupata
huduma kwa mwaka mzima.
" Ndugu zangu wananchi wa Kata ya Nyamatare mkutano wetu wa
leo pamoja na mambo mengine lakini tunautumia kuhamasishana umuhimu wa kupata
afya bora.
" Tusisubili kuugua tukaanza kuangaika kutafuta fedha za
kwenda kujitibu naomba kila mmoja achukulie umuhimu na kuwa na kadi ya
kuwezesha kutibu pamoja na familia,"amesema Masumbuko.
Akizungumzia masuala ya urasimishaji wa ardhi,diwani huyo
amesema Kata ya Nyamatare ipo kwenye mpango wa kuwapimia ardhi wananchi na
kuwaomba wananchi kuwapa ushirikiano wataalamu watakaofika kwenye maeneo hayo
kwaajili ya zoezi hilo.
Kwa upande wa elimu amesema maboresho yameendelea kufanyika
kwenye shule ya msingi Nyamatare kwa kukarabati majengo 4 ya madarasa na bado
kuna majengo mengine 4 ambayo ushirikiano unahitajika ili kuweza kuyanaliza na
kuwapa wanafunzi kusoma kwa nafasi.
Diwani Masumbuko (kulia) akiwa na Katibu wa CCM Kata ya Nyamatare,Rashid Mohamed |
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyamatare akifungua mkutano huo |
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Nyamatare, Mwamini Salum akizungumza kwenye mkutano huo
Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano
No comments