Wanajeshi wa Makoko wapigishwa kwata kombe la diwani
TIMU ya soka ya kikosi cha 27 Makoko kilichopo manispaa ya Musoma imepigishwa kwata na timu ya Nyarigamba FC na kukubali kichapo cha mabao 2-1 katika mashindano ya kombe la diwani yaliyoanza kutimua vumbi juni 3 kwenye uwanja wa shule ya msingi Nyarigamba na kuzishirikisha timu 10 za Kata hiyo. Akifungua mashindano hayo,diwani wa Kata ya Makoko ambaye pia ni Meya wa manispaa ya Musoma, William Gumbo, amesema mashindano hayo yana lengo la kujenga mahusiano na kuinua vipaji ambayo yameanzishwa na ofisi ya kata kwa kushirikiana na ofisi yake. |
HII picha ya makataba, Diwani wa Kata ya Makoko, William Gumbo, akikabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Musoma,Dk.Vicent Naano, tuzo baada ya kuiisaidia timu ya Biashara United kupanda ligi kuu msimu ujao |
No comments